0

Tiffa Dangote mwanao Diamond Platnumz pamoja na Zari aliingia duniani wiki jana na chini ya masaa  ishirini na nne aliangukia deal ya mamilioni. Mbali na deal ya mamilioni, umaarufu kwenye mtandao ndicho kilicho ambatana na kuzaliwa kwake. Thibithisho ni akaunti yake ya instagram ambayo hadi sasa imepata followers zaidi ya 70,000.

Diamond hakusita kuonyesha furaha yake kupitia picha za Tiffa ambazo  aliziweka  kwa mtando kwa wingi. Kama kawaida drama hazikosi kumfuata Zari. Drama ya hivi punde ni madai ya jamaa mmoja anayeitwa King Lawrance ambaye pia ni rafiki wa Karibu wa aliyekuwa mumewe Zari. Alichokisema Lawrance ni kuwa yuko na ushahidi kuwa Tiffa Dangote sio mwanawe Diamond. King Lawrance ambaye kipindi fulani alimuita diamond kuwa yeye ni Zari's Toy Boy, aliweka picha zifuatazo kwenye mtando:


Chilling with @princess_tiffah’s father

No DNA Needed. The best revenge has shown itself after 9months. 

King Lawrance anadai kuwa Tiffa Dangote ni mtoto wa aliyekuwa mumewe Zari.

Kwa mtazamo wangu kinachomuuma King Lawrance ni machungu tu kuhusu uhusiano wa Diamond na Zari. Anachostahili kufanya ni kujihusisha na mambo ambayo huenda yatamjenga maishani kuliko kujihusisha na vitu visivyo na msingi wowote. Kinachosubiriwa zaidi ni namna Zari pamoja na Diamond watayachukulia madai haya.

Post a Comment

 
Top