0

Anaitwa Rose Muhando, mwanadada ambaye amewagusa na kuwabadilisha wengi waliopotea kwa dhambi kupitia nyimbo zake zenye mafunzo. Rose alizaliwa mnamo mwaka wa 1976 katika kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, maeneo ya Morogoro nchini Tanzania.

Tangu abadilishe dini maisha yake yamekuwa na matatizo hususan kwenye safari yake ya muziki ambapo amekumbwa na scandal nyingi ambazo zimemwathiri pakubwa. Hivi majuzi kulikuwa na uvumi kuwa, aliavya mimba kitu ambacho alikana na kusema kuwa huko ni kusingiziwa tu.

Itaeleweka kuwa Hitmaker huyo wa Facebook ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kupewa mkataba na kampuni ya Sony vile vile nyimbo zake kuchezwa na Vevo. Hatua hii iliwafanya watu kuanza kumhusisha na maswala ya illuminati

Ni kawaida kwa kila binadamu kupitia majaribu maishani kwa kuwa majaribu ndiyo yamwandao binadamu kwa maisha bora ya kesho. Huenda ikawa hali hiyo ngumu ndiyo humsababisha Muhando kuimba nyimbo ambazo huwagusa na kubadilisha wengi.

Kwa sababu ya matatizo ambayo yamekuwa yakimsibu, Rose ameamua kujislimisha na kuuasi ukristo. Ninacho kijua ni kuwa kubadilisha dini haitakuwa suluhu ya matatizo yake. Kikubwa ambacho Rose Muhando anafaa kukifanya ni kuzidisha maombi na mwisho wa siku najua Mola hamsahau mja wake.

Post a Comment

 
Top