Mbali na kushinda tuzo ya Best live act,
hiyo jana Diamond platnumz aliangusha bonge la show na msanii Flavour ambapo waliimba hit yao ya nana. Ushindi wa diamond platnumz, unaitangaza vizuri muziki wa Afrika Mashariki na hivyo kufungua njia kwa ufanisi wa wasanii wengine. Hit maker huyo wa Nitampata wapi alikuwa na haya kwa mashabiki wake kwenye mtandao wake wa Instagram
“Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote #TeamWasafi kwa kunipigia kura na Kuhamasisha kwa Nguvu,”
Katika ukarasa wake wa facebook diamond alikuwa na haya ya kusema:
"Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote kwa kunipigia kura na Kuhamasisha kwa Nguvu...Niushkuru sana Uongozi wangu, Familia pamoja na Team nzima ya @wcb_wasafi hususan Madancers wangu kwani Naamini wao ndio wamenipika nikapikika hadi leo hii kuweza kuletaTunzo hii Nzito ya Mtumbwizaji Bora Africa, Nyumbani...lakini pia Shukrani za kipekee zimfikie Mama yangu kipenzi Sandra kwa Mafunzo na Malezi anayonipa kila siku juu ya Dunia....na Shukran tena za kipekee na aina yake zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu @zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa M'bunifu kwenye kazi..🙏#BestLiveAct #Mtvmama2015 Asanteni sana" 🙏
Diamond akiwa na meneja wake Babu Tale baada ya kuchukua tuzo |
Vile vile Diamond hakusita kurudisha shukran za dhati kwa mpenzi wake Zari The Bosslady
“Na Shukran tena za kipekee na aina yake zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu @zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa M’bunifu kwenye kazi.. #BestLiveAct .
Wanaijeria ndiwo waliotawala tuzo hizo, tazama washindi wote hapo chini:
Best Female: Yemi Alade (Nigeria)
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Group: P-Square (Nigeria)
Best New Act Transformed by Absolut: Patoranking (Nigeria)
Best Hip Hop: Cassper Nyovest (South Africa)
Best Collaboration : AKA, Burna Boy, Da LES & JR: “All Eyes On Me” (SA/Nigeria)
Song of the Year: Mavins: “Dorobucci” (Nigeria)
Best Live: Diamond Platnumz (Tanzania)
Video of the Year: “Nafukwa” – Riky Rick; Director: Adriaan Louw Best Pop & Alternative: Jeremy Loops (South Africa)
Best Francophone: DJ Arafat (Ivory Coast)
Best Lusophone: Ary (Angola)
Personality of the Year: Trevor Noah (South Africa) MAMA Evolution: D’Banj (Nigeria)
Best International: Nicki Minaj Artist of the Decade: P-Square MTV Base Leadership Award: Saran Kaba Jones & S’Bu Mavundla.
Post a Comment