Hivi unajua majina kamili ya wasanii unaowapenda wa Afrika Mashariki?
Siku zote usilolijua ni usiku wa giza ndio
maana nimeamua kukuandalia makala ya kuwatambua wasanii unaowapenda kwa majina yao halisi. Majina yao ya usanii au a.k.a huwapatia mashabiki uepesi wa kuwakumbuka.
Juacali
Ni mmojawapo wa wasanii ambao wamechangia sana muziki wa Genge nchini kenya. Inakisiwa kuwa Calif records anaimiliki yeye pamoja na producer Clemmo. Jina lake ni Paul Ndunda.
Size 8 Reborn
Huyu naye ni msanii ambaye amefanya wengi wakajua kuwa maishani chochote kinawezekana. Kabla ya kuamua kuchukua mkondo tofauti wa maisha alikuwa na maisha ambayo yaliwashangaza wengi sana. Utulivu wake kwa ndoa umemfanya apate heshima zaidi nchini Kenya. Jina lake ni Linet Munyali Masivo.
Octopizzo
Huwezi kutaja Hip hop nchini kenya bila kumtaja Octopizzo namba nane. Huyu ni msanii ambaye ametoka mbali na bidii yake ya mchwa zimemsababisha kukubalika zaidi nchini Kenya na ulimwengu mzima. Jina lake ni Henry Ohanga.
Rabbit Kaka Sungura
Mistari yake yenye mnato na mvuto imemfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wanaopendwa nchini Kenya. Kaka Empire ndiyo kampuni aliyoianzisha hivi karibuni na kampuni ambayo inasimamia wasanii wengi mmoja wao ni Rich Mavoko toka Tanzania. Jina lake ni Kennedy Ombima.
Pilipili
Sauti yake tamu ambayo ndiyo anayoitumia kama chambo cha kuwanasa mashabiki wake. Alikuwa miongoni mwa wasanii walioweka msingi thabiti kwa nyimbo za kizazi cha sasa nchini Kenya. Jina lake ni Peter Gatonye.
Susumila
Susumila alitumia mbinu ya kipekee kuiteka anga ya Afrika Mashariki. Alianza kwa kuwasuta wasanii na nyimbo zake za awali kama vile siasa duni. Jina lake ni Yusuf Kombo.
Diamond Platnumz
Huyu ndiye msanii anayependwa zaidi Afrika Mashariki kutokana na nyimbo zake zenye uepesi kuimba na kusalia akilini mwa mashabiki wengi. Jina lake ni Abdul Naseeb.
Sudi Boy
Ukiachana na mvuto wake ambo huwaacha wasichana hoi, huyu ni msanii ambaye nyimbo zake huburudisha na kukonga nafsi za mashabiki wengi. Hitmaker huyu wa Barua kwa rais jina lake ni Ricky Bekko.
Jaguar
Ni msanii mwenye moyo wa kasaidi hasa wale wenye tabaka la chini maishani. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri ndiyo methali inayomwongoza kila wakati akisaidia jamii. Hitmaker huyu wa Huu mwaka jina lake ni Charles Njagua.
Naamini sasa angalau umejua majina kamili ya baadhi ya wasanii ambao unawapenda Afrika mashariki . Wengine watafuatia kwa makala amabayo yatachapishwa sio kitambo.
Post a Comment