0

Ikiwa umekuwa ukifuatilia kwa makini runinga ya KTN basi bila shaka mtangazaji Mwanaisha Chidzuga sio mgeni kwako. Sauti yake ya kipekee na  mtiririko mzuri wa lugha ya kiswahili ndivyo vitu ambavyo humweka kipao mbele kwenye ulingo wa utangazaji.

Habari ya kuhuzunisha ni kuwa Mwanaisha  ameachishwa kazi. Kampuni ya standard Group amabyo pia inamiliki kituo cha runinga cha KTN, imewaachisha watangazaji wengi kazi kama njia moja ya kujaribu kupunguza gharama ya matumizi. Makali ya hatua hii haikumsaza mwanadanda huyu ambaye ni kipenzi cha wengi.

Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika imedhihirisha kuwa sasa hivi Mwanaisha Chidzuga anafanya kazi kwenye mkahawa fulani ambao upo takriban mita 200 kutoka kwa pahali makao makuu ya kampuni ya Standard Group.

Post a Comment

 
Top