0

Msanii Hubert Nakitare maarufu kama Nonini, ni mmojawapo wa wasanii walioweka msingi thabati kwa sanaa ya burudani nchini kenya. Kama anavyojiita Mgenge 2ru siku zote amekuwa mwaminifu kwa mashabaiki wake kwa kuwaburudisha na kuwagusa.

Mbali na burudani Nonini sio mchache wa kuisaidia jamii. Kampaini yake ya Colour kwa face ambayo inalenga kutetea haki za Mazeruzeru imempatia heshma sio tu nchini bali pia Duniani. Kama njia mmoja ya kutambua juhudi zake, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini (Safaricom) imemkabidhi shillingi 404, 980. Pesa hizi zitamwezesha Nonini kuendeleza kamapeni yake ya Colour kwa face.


Post a Comment

 
Top