0
Image result for alikiba NA DAVIDO
Ni dhahiri kuwa mafanikio makubwa anayoyafurahia msanii Diamond Platnumz yalitokana na
collabo yake ya wimbo  wa  Number one remix alioufanya na Davido .  Habari njema ni kuwa mshindi wa tuzo za MTVMAMA2015 kitengo cha Male Artist of the Year kwa miaka miwili mfululizo David Adeleke maarufu kama Davido, amethibithisha kuwa amefanya wimbo na Alikiba.

Akizungumza na mtangazaji mashuhuri nchini Tanzania Millard Ayo katika Red carpet ya MTVMAMA2015, Davido alikuwa na haya ya kusema:
“I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy”
Alikba naye alikuwa na furaha baada ya kupata habari hiki ndicho alichokiandika kwenye mtandao wake wa instagram:
"Inshalla@davido lets do this for Afrika!!! Asante"

Bila shaka hii ndiyo collabo inayosubiriwa zaidi na mashabiki wa muziki wa kizazi cha sasa.

Post a Comment

 
Top