Hii ndio sababu rais Obama aliacha zawadi ya uchoraji na kinyagu(sculpture) aliyopewa na rais Uhuru Kenyatta
Siku zote mgeni akitembelea wenyeji ni vyema apewe zawadi ambayo itamkumbusha safari yake. Kwa muujibu wa msemo wa zama, mbuzi wa kupewa haangaliwi kama ana pengo ndio maana
chochote unachopewa kama zawadi ni vyema kukipokea. Zawadi ya uchoraji na uchongaji aliyopewa rais barack Obama haukuichukua. Kazi yenyewe ya uchoraji ilikuwa imefanywa na Collins Okello.
Sababu iliyomfanya rais Obama kutochukua zawadi ni kuwa sheria za marekani hazimruhsu kupokea zawadi ya aina yeyote ile kutoka kwa kiongozi wa taifa lingine. Ili rais apokee zawadi lazima ipitie na ikaguliwe kwa idara inayohusika na maswala ya zawadi za kiongozi wa taifa.
Rais wa marekani huruhusiwa tu kupokea zawadi kutoka kwa familia yake au raia wa marekani. Hata hivyo msimamizi wa maswala ya udijitali ya ikulu bwana Denis Itumbi, ameiambia gazeti la Taifa kuwa utaratibu unaofaa kufuatwa ili kumpokeza rais Obama zawadi yake umeanza.
Collins Okello ambaye ndiye aliyechora picha hiyo alipata umaarufu kipindi kile alipomchora rais Uhuru Kenyatta akiwa amevalia gwanda la kijeshi.
Post a Comment