Mara nyingi mwanamke ambaye amejifungua mtoto huchukua muda mrefu kabla ya kurudisha umbo lake linalotamanisha. Kinyume na hali hii, Zari the Boss Lady haikumchukua muda mrefu ili arudishe umbo lake lenye mvuto baada ya kujifungua Tiffa Dandote.
Swali ni, je kipi alichokifanya Zari? Huenda utadhani kuwa ni ilkuwa kazi rahisi lakini ukweli ni kuwa ilimbidi Zari asimnyonyeshe mwanae ili arejeshe umbo lake. Diamond Platnumz ndiye aliyefichua madai hayo huku akisema kuwa mwanao amekuwa akipewa maziwa ya ng'ombe.
Hali hii inaonyesha kuwa Zari amekuwa akifuatilia sana Kurudisha umbo lake kuliko kumlea mwanae. Hata hivyo mbali na mama Tiffa kutompa mwanae maziwa, ameonekana mara nyingi akipost picha akiwa Gym hali amabayo bila shaka imechangia Umbo lake kuboreka zaidi.
Post a Comment