Mwezi wa nane siku zote huwatatiza wakenya sana hasa kwa kuwapoteza wapendwa wao. Kisa cha hivi punde ni wanafunzi kutoka shule ya msingi ya St. Martin ambao walizama maji wakati wakipiga mbizi maeneo ya Pavilion Beach katika kaunti ya Kwale.
Inadaiwa kuwa mawimbi ya bahari yaliwatatiza sana hadi yakawasababisha wanne hao kuzama. Kisa hiki kilifanyika majira ya saa kumi na moja jioni siku ya jana. Kamishna wa kaunti bwana Evans Achoki alisema kuwa juhudi za kuwatafuta wengine wanne zinaendelea huku ikihofiwa kuwa huenda pia hao wameangamia.
Wanafunzi hao pamoja na wenzao 56 walikuwa katika ziara ya kuzuru Bahari Hindi amabayo walitoka shuleni tarehe 7 agosti na wangerejea shuleni mwao tarehe 13 ijumaa ya kesho.
Mili ya wanafunzi hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Diani District.
Post a Comment