0

Mwimbaji wa Marekani Shaffer Chimere Smith maarufu kama Neyo, yuko mbioni kulitembelea taifa la kenya. Mshindi huyu wa tuzo za Grammy, ni mmojawapo wa wasanii ambao wanapendwa zaidi duniani kwa sababu ya sauti yake tamu yenye upekee wa aina yake.

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika imedai kuwa Neyo atazuru kenya ili kuhudhuria msimu wa tatu wa Coke Studio Afrika. Awali jitihadha za Coke Studio Kumleta mwimbaji John Legend, hazikufua dafu, kwa sababu ya ratiba yake ambayo haingemwezesha.

Mwaka huu Coke Studio Afrika, imewaunganisha wasanii wenye vipaji kutoka mataifa kama vile Kenya, Tanzania, Uganda, Nigeria pamoja na Mozambique.

Post a Comment

 
Top