0

Bibilia takatifu husema kuwa "omba nawe utapewa", msanii Charles Njagua maarufu kama Jaguar alifanya hivyo na bila shaka amepewa. Mwanzoni mwa mwaka huu alitoa wimbo ambao unaitwa Huu mwaka, ndani ya huo wimbo, kuna mstari ambao  unasema kuwa, huu mwaka lazima nipate. Namna hali ilivyo ni kuwa ameshapata.


Sherehe ya nane ya kufuzu kwa mahafala wa chuo kikuu cha Mount Kenya zilifanyika hii leo. Jaguar ni mmojawapo wa watu waliopewa shahada. Mbali na kupewa shahada, jaguar alipewa rasmi kazi ya kuwa balozi wa chuo kikuu hicho. Kupitia ukurasa wake wa facebook, alikuwa na haya ya kusema:
"New heights everyday...thanx Mount kenya university for making me ur Goodwill ambassador."



Post a Comment

 
Top