0

Tume ya kuwaajiri waalimu nchini TSC  imeamua kufanya kitu ambacho itakitumia kama njia moja ya kukwepa amrisho la mahakama kuhusu kuwaongezea waalimu mishara yao. Itafahamika kuwa TSC imeamrisha  mara mbili na mahakama ili iwaongezee waalimu mishahara yao kwa asilimia 50-60 ambapo nyongesa hiyo ingefaa kuanza mwezi huu wa agosti.

Kinyume na kawaida, TSC iliamua kulipa mishahara ya walimu mnamo tarehe 22 mwezi huu wa nane. Hii ni  mapema sana ikilinganishwa na tarehe za hapo awali, ambapo tume hiyo imekuwa ikilipa misahara ya walimu. Hatua hii imeonekana kama mbinu mpya ambayo TSC inataka kutumia ili kukwepa agizo la mahakama.

Mahakama inafaa kutoa uamuzi wa mwiso tarehe 24 mwezi huu wa nane kuhusu mzozo huu unaohusu nyongesa ya mishahara ya walimu  Mwenyekiti wa kitaifa wa  KUPPET bwana Omboko Milemba alikuwa na haya ya kusema:
“If the court rules in our favor, they (TSC) will start saying that they have already paid teachers and therefore cannot include the increment in the August salaries,” 

. Bwana Omboko aliongeza kusema kuwa:

“They always delay our salaries and when they decide to pay us on time it is not because they care, they are doing it for their own benefit,”

Tayari chama cha waalimu KNUT kimetishia kuitisha mgomo muhula wa tatu utakapoanza endapo waalimu hawataongezewa mishahara yao.

Post a Comment

 
Top