Ukweli hauwezi ukafichika hata iwe vipi. Ni hivi majuzi tu ambapo msanii maarufu bahati alimkashifu msanii mwenzake Daddy Owen, kwa kutomfanyia haki msanii mwenzake Denno. Hii ilibainika wazi baada ya maswali mengi kujitokeza kuhusu hali duni ya maisha ya msanii Denno, ambaye alichangia pakubwa wimbo wa Mbona wakishirikiana na Daddy owen.
Kama njia moja ya kujaribu kumrudisha na kumpa moyo msanii huyo mlemavu Denno, Bahati aliamua kufanya naye Collabo inayoitwa stori yangu ambayo imepokelewa vizuri.
Hata hivyo Daddy owen aliamua kunyamaza bila ya kujibu lolote. Mambo yalionekana kumharibikia Daddy Owen zaidi baada, Denno kukiri kuwa, hakupata manufaa yoyote kutokana na wimbo huo wa Mbona.
Denno and Bahati |
Kinyume na hali ilivyo bodi inayoshughulikia nyimbo za wasanii nchini MCSK, imejitokeza na kusema kuwa madai ya Denno sio ya kweli kwa sababu rekodi zinaonyesha kuwa Denno alipewa royalties na vituo vya redio na Tv,kutokana na wimbo wa mbona. Hali hii imedhihirisha kuwa kashfa ambazo msanii Bahati alizielekeza kwake Daddy Owen sio za kweli.
Mimi sisemi kitu kile ninachojua ni, kuwa ukweli ukidhihirika uongo hujitenga. Acha tusubiri tuone namna mambo yatakwenda.
Post a Comment