Mojawapo wa ugonjwa ambao unaogopwa sana kwa hii karne ni Ukimwi. Watafiti hawalali wala kusinzia huku juhudi zote zikielekezwa kwa kupambana na ugonjwa huu.
Hatua nyingi zimepigwa ila iliyopigwa hivi karibuni ni uzinduzi wa mpira wa kondomu ambao upo na uwezo wa kuuwa virusi vya ukimwi na vile vile kuongeza utamu zaidi hasa wakati wa tendo la ngono.
Hii imetokana na bidii ya wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Texas A&M Health Sciences. Kondomu hizo zitapatikana dukani kuanzia mwakani na utauzwa takriban dola moja.
Post a Comment