1982. Majina yake kamili ni Ambwene Yesaya. Ikiwa leo ni tarehe yake ya kuzaliwa yafwatayo ndiyo aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa facebook:
July 5, 1982 Ambwene Yessayah alizaliwa. Namshukuru Mungu kwa kuiona siku hii ya leo. Nawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani. Mungu awalaze mahali pema peponi. Natamani mama yangu angekuwa hai aone jinsi kijana wake alivyokuwa mkubwa na pengine afurahie jasho lake la kunizaa, kunilea na kunitunza.
Nawashukuru wote walio na mchango mkubwa kwenye maisha yangu, ni wengi siwezi kuwamaliza kuwataja. Navikushukuru vyombo vya habari vyote kwa support kubwa inayoendelea kunipa. Nakushukuru pia wewe shabiki yangu kwa kuendelea kuniunga mkono. Thank You!!
Nami nimeona ni bora kwa utaratibu nikuandalie makala ya baadhi ya wsanii amabo A.Y amechangia pakubwa sana kwenye ufanisi wao kwa sanaa ya muziki
1. Jaguar
Charles Njagua maarufu kama Jaguar ni mojawapo wa wasanii ambao msingi wa ufanisi wake uko chini wa mwavuli wa A.Y. Hitmaker huyo wa huu mwaka ni mojawapo wa wasanii ambao wamefanya vizuri Afrika Mashari na hata Afrika kwa ujumla. Wimbo amabao ulimpa Jaguar umaarufu zaidi ni NIMETOKA MBALI ambao alimshirikisha hitmaker wa ZIGO. Nimetoka mbali ulitawala chati za Afrika mashari kwa muda mrefu na bila ubishi uwepo wa A.Y kwenye wimbo huo ulifanya wimbo huo kufanya vyema zaidi
2. Wahu Kagwi
Wahu ni mwanamziki ambaye mbali na kuwa msanii yeye pia ni mzazi aliyejaliwa na watoto wawili yeye pamoja na mwanamuziki David Mathenge maarufu kama Nameless. Mchango wa ufanisi wa A.y kwa ufanisi wa Wahu unatokana na collabo ambayo alimshirikisha remix ya wimbo wake LEO wimbo ambao ulifanya vizuri Afrika mashariki. Isitoshe A.Y alimshirikisha Avril kwenye remix ya wimbo huo huo wa LEO
3. DIAMOND PLATNUMZ
Katika ujumbe ambao Diamond platnumz aliundika kwenye INSTAGRAM haya ndiyo aliyoyasema kuhusu A.Y:
Misingi na Daraja Imara la kimataifa ulio tujengea na unayozidi kutujengea ndio leo inatusaidia vijana wako nasi kuweza kupenyeza na kutangaza kazi zetu kimataifa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pengine watu hawajui kuwa wewe ndio uliyeniwezeshea kufanikisha Collabo langu na Davido, Kuniunga na Godfather na vingi ambavyo naamini ndio Mwanzo wa safari yangu ya Kimataifa… Nakuheshim sana Brother, na daima nitahakikisha sikuangushiemoji…Happy birthday Bro.”
Vilevile Diamond aliongeza kusema kuwa A.Y ndiye aliyefanikisha collabo ya NUMBER ONE REMIX pamoja na Davido na bila shaka huu ndio wimbo uliomtangaza vizuri kimataifa. Itaeleweka kuwa A.Y pia ndiye aliyemuunganisha na mtayarishi wa video kutoka Afrika kusini Godfather.
Post a Comment