Ni matarajio ya kila mtu kutangamana na kiongozi anayelindwa zaidi duniani, rais Barack Obama. Mapokezi aliyoyapata baada ya kufika kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ulikuwa wakipekee, hasa ikizingatiwa kuwa
alikaribishwa na msichana mdogo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka minane, anaitwa Joan Wamaitha, mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi ya Mariakani inayopatikana eneo la South B, Nairobi. Joan Wamaitha ni yatima na anlelewa kwa makao ya watoto yatima ya Mama Ngina.
Rais Obama akipigwa picha na Joan Wamaitha |
Pindi tu baada ya kushuka kutoka kwa ndege, wengi walitarajia kuwa Rais Uhuru Kenyatta ndiye angekuwa wakwanza kumsalimia lakini kinyume na matarajio, Joan Wamaitha ndiye aliyefanya hivyo. Makaribisho hayo yalikuwa yakipekee na pia yenye kusalia akilini mwa wengi.
Moja wa walimu wake kwa jina Bi Pauline Musyoka alishangaa sana kumwona na hakujua kuwa mmoja wa mwanafunzi wake alikuwa amechaguliwa kumkaribisha rais Brack Obama kwa shada la maua. Bi Pauline aliongeza kuwa Joan Wamaitha ni mtoto mwerevu sana darasani.
“She is one the brightest pupils in her class,”
Post a Comment