Hali ilivyo ni rasmi kuwa rais wa Marekani Barack Obama atazuru chuo kikuu cha Kenyatta. Awali wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi walitoa vitisho endapo Rais Barack Obama angekosa kuitembelea chuo hicho huku wakisahau kuwa,
kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji. Rais Barack Obama yupo nchini Kenya kuhudhuria Kongamano la ujasiriamali amabalo litafanyika hii leo maeneo ya Gigiri.
Kama njia moja ya kuwatayarisha wanafunzi kumpokea na kumkaribisha chuoni rais Barack Obama siku ya Jumapili asubuhi, profesa Olive Mugenda aliandaa mkutano wa dharula ambapo alizungumza na wanafunzi kwenye ukumbi wa Amphitheatre.
Profesa Olive Mugenda |
Kwenye hotuba yake, naibu chansela alisema kuwa Jumapili asubuhi wanafunzi watapanga foleni kutoka kwa njia ambayo inatoka lango la Amphitheatre hadi kwa idara ya Jiografia(Geography department) huku mkononi wakibeba bendera ya kenya au marekani. Aliongeza kuwa usalama utapewa kipao mbele huku maafisa wa usalama chuoni, wa kitaifa pamoja na wale wa marekani watachukua usukani.
Kikubwa ni kuwa wanafunzi wanafaa kubeba vitambulisho vyao ili kupunguza mikwaruzo biana yao na maafisa wa usalama.
Profesa aliongeza kuwa ujio wa rais Barack chuoni kuna manufaa mengi kwa kuwa ni kitu cha kihistoria na itakuwa ni kama kuweka chuo kikuu cha kenyatta kwenye upeo mzuri duniani. Halikadhalika alieleza kuwa njia atakayotumia rais huyo ni ile inayotoka kwa ukumbi wa Amphitheatre hadi kwa idara ya Jiografia.
Post a Comment