Wasanii wengi walifanya vizuri enzi ya nyuma na ikiwa walifanya vizuri inamaanisha
kuwa uwezo wao bado ulikuwa mkubwa. Japo sanaa inabadilika kila kuchao ni jukumu la msanii kusoma namna soko la muziki linavyobadilika. Nimeamuwa kukuandalia makala ya wasanii mbao walifanya vizuri miaka ya nyuma na wameshindwa kurudi tena kwenye "Game".
KALAMASHAKA
Kwa jina lingine K-Shaka ni kundi la hip hop lenye makao yake katika mtaa wa Dandora, kitongoji katika mji wa Nairobi, Kenya. Kinajumuisha wasanii watatu: Oteraw, Kama na Johny. Kikundi hiki kiliundwa katika miaka ya katikati ya 1990. Walikuwa maarufu kwa wimbo wao Tafsiri Hii uliovuma sana mwaka wa 1997. Kundi hili lilifungua pazia kwa wasanii nyota kadhaa wa kimataifa kati yao Coolio na Lost Boyz na wameimba pamoja na Dead Prez na wasanii wengine wa kimataifa. Wametumbuiza katika nchi kadhaa kama vile Nigeria, Uswidi, Uholanzi, Afrika Kusini, Norway miongoni mwa nyingine. Kalamashaka walifungua njia kwa hip hop katika lugha ya Kiswahili na ikawa inatawala nchini Kenya. Kikundi hiki ni maarufu na mashabiki wake kwa muziki wake wa hardcore rap na wenye ujumbe wa kijamii na kisiasa. Albamu yao ya kwanza Ni Wakati iliyotolewa mwaka wa 2001 ilivuma sana na Channel O ya Afrika Kusini ilicheza mmoja ya video "Fanya Mambo" kutoka katika albamu hii. Albamu hii iliangazia uhalifu mitaani, ukabila, siasa na migogoro ya Afrika. Umaarufu wao ulianza kupungua wakati mitindo ya Genge na Kapuka ilipoibuka ambayo ilikuwa inaweza kuchezeka kwa urahisi na yenye tasfoa ambayo asilimia kubwa ya vijana wanapendelea kusikiliza kuliko muziki wa kifalsafa. Stesheni za redio za FM husita kucheza miziki yenye mpigo wa kijamii kama unaochezwa na Kalamashaka na kupelekea kupungua kwa umaarufu wao. Hata hivyo, kikundi hiki kimeendelea kufanya kazi na kukataa kubadili mtindo kulingana na nyakati na kufanya biashara ya muzik. Kundi hili lilisukuma makundi mengine kama Mashifta, Gidi Gidi Maji Maji, K-South, Necessary Noize na wasanii wengine wengi.
Uwezo wao wa kufoka ulikuwa mkubwa sana na ni ishara kwamba endapo wanaweza wakajiandaa vizuri na kusoma kile soko la muziki linahitaji sasa hivi wanaweza wakarudi na bado wakakubalika kama walivyo kuwa wamekubalika hiyo zamani.
Flexx
Majina yake kamili anaitwa Micheal Mwangi na ni moja wapo wa wasanii ambao tasnia ya burudani nchini kenya ilitegemea sana miaka ya hapo nyuma, Flex ndilo jina ambalo analitumia kwenye Game. Baada ya kuhit na Ngoma kama vile Nyundo, Amejibeba, kama wanitaka na pia Namba yako aliamua kuhamia nchini Sweden. Flexx ni jina alilopatiwa na Clemmo mtayarishi na vile vile mmiliki wa studio ya calif records, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kuimba style nyingi zikiwemo raggea, ragga, genge kapuka, miongoni mwa zingine.
Habib Namanga
Habib ni ndugu wa toka nitoke wa marehemu E-sir mmari amabaye alikuwa mmojawapo wa wasanii walioweka msingi thabiti katika ulingo wa muziki Afrika mashariki. Nyimbo ambazo zilimpa jina Habib ni Bata pamoja na Fever na ni dahiri kuwa nyimbo hizi zilifanya vyema zaidi.
Uwezo wa habib ni mkubwa sana na bila shaka inamaanisha kuwa anaweza akarudi na akafanya vizuri hata katika soko la sasa kwa muziki.
C'ZARS
Alionekana mara ya mwisho mnamo tarehe 13 mwezi wa oktoba mwaka wa 2006, na huo ndio wakati ambao kapaji chake kilikuwa kimeteka anga ya afrika mashariki. Amka ukatike niwimbo alioumba na ulifanaya vizuri sana na alikuwa fahari kubwa kwa wazazi wake na vile vile wakaazi wa mombasa.
Juhudi za kumtafuta zimeambulia patupu na hata wazazi wake wamejaribu kutoa pesa nyingi kwa yeyote atakaye toa habari yoyote kuhusu pahali alipo. Babake Abdulkarim Makasi amekuwa na wakati mgumu hasa asijue ikiwa mwanawe yuko hai ama ameaga dunia. Ni uchungu sana kwa mzazi yeyote yule kukosa kumwona mtoto wake hususan wakati unashindwa kujua ikiwa yuko hai ama ama ameenda jongomeo. Maombi ya kila mtu ni kuwa siku moja C'zars atarudi nyumbani akiwa hai na furaha itarejea tena kwa familia ya Makasi.
Nasty Thomas
Nasty Thomas pamoja na Colonel mustafa ndiwo wasanii waliounda kundi la DUEX VULTURES ambalo lilitamba na ngoma kama vile Adhiambo, Monalisa na Katika wimbo amabao walishirikisha kundi la Longombaz.
Jina lake halisi ni Thomas Konzanga na ni msanii amabye akiwa mdogo aliishi nchi jirani ya Tanzania. Baada ya kufanya vizuri Kimziki aliamua kuende kuishi nchi ya Norway na mwaka wa 2013 alisema kuwa hayuko tayari kurudi Kenya hivi karibuni.
Wasanii amabao walifanya vizuri ni wengi na leo nimeamua kukutajia tu hao wachache. Ikiwa msanii ana uwezo wa kuimba inamaanisha kuwa ana talanta, na kikubwa ambacho anafaa kufanya ni kuona namna soko la muzikil linavyobadilika.
Post a Comment