0

Jehova Wanyonyi ni kiongozi vilevile mungu wa kundi fulani la waumini linalojiita Israel Sect. Hivi majuzi habari ilivuma kuwa alikwa amefariki dunia, kitu ambacho kilisababisha waumini wake kuingiwa na hali ya hofu. Wanyonyi Anaishi Nangili mpaka wa kaunti ya Uasin Gishu na ile ya Kakamega.

Idadi ya waumini wake ni Zaidi ya 1000 ambao wanatoka taifa la Kenya na lile la Uganda. Msemaji wa familia bwana Eliab Masinde alikuwa na haya ya kuliambia gazeti la Star:


“We know he is with his sons at a hospital in Nairobi where they are taking care of him…he is not dead and we will make information about him available soon,”

Jehova wanyonyi yuko na wanawake 25 na watoto 95. Aliwahi sema kuwa yeye ndiye mungu wa kweli na aliamua kuja duniani baada ya binadamu kumpuuza mwanawe Yesu Kristo.

Waumini wake wamekuwa wakipiga kambi nyumbani kwake Nangili tangu 17 julai, 2015, wakati ambapo iliripotiwa kuwa alikuwa amepotea.

Post a Comment

 
Top