0

Pastor James Maina Nganga aligonga vichwa vya habari baada ya kukisiwa kuwa, alimuuwa Mercy Njeri na kumjeruhi vibaya bwana yake kufuatia kwa kile kilitambulika kama matumizi mabaya ya barabara. Kisa hiki kilifanyika katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi, japo muhubiri huyo wa Neno Evangelism amekana madai hayo.

Miongoni mwa kitu ambacho kiliwashangaza wengi ni vitu ambavyo vilipatikana ndani ya gari lake aina ya Range Rover. Polisi walifanyia upekuzi wa kina gari hilo na miongoni mwa vitu vilivyopatikana ni: nguo za ndani zililzokuwa zimekolea uchafu, mipira ya kondomu ambao imetumika na chupa za pombe.

Ikiwa wenye jukumu la kuendeleza injili ya kutubu na utakatifu ndio wanahusika kwa maswala ya kufedhehesha, hivi ni nani ataikomboa dunia? Jibu unalo mwenyewe. Fanya mema na wema utakufuata. Ni kweli kuwa hamna aliyemtakatifu mbele za bwana lakini ni vyema wanaojivisha taji la mhubiri kuongoza kwa vitendo.

Post a Comment

 
Top