0
Clarice
Siku zote tuzo aina yoyote kwenye ulingo wowote ni kitu ambacho mbali na kumpa mshindi moyo wa kutia bidii vilevile huonyesha namna vipaji vinapewa kipau mbele. Tuzo za Nollyhood  & African People's Choice Awards ambazo vilevile huitwa African Oscars awamu ya tano zilitangaza washindi wake.

Miongoni mwa washindi wakubwa ni mchekeshaji wa Uganda Anne Kansime (‘Favorite Comedian’) ambaye aliwashinda vigogo wakubwa kama vile Klint The Drink pamoja na Basket Mouth. Diamond Platnumz vilevile alikuwa na sababu kubwa ya kutabasamu baada ya kushinda tuzo mbili ‘Favorite song na Favorite artist of the year’.  Kufuatia ushindi huu Diamond aliwashukuru mashabiki kupitia ukurasa wake wa facebook:

"Thanks alot to my all Fans around the World, for your unconditional love and Support that you been Giving me... i can't even explain how grateful i am... two awards on NollyWood & African People Choice Awards"



Taifa la kenya nalo halikutoka bure kwa kuwa muigizaji Clarice Otieno, mwenye umbo la mvuto alijishindia tuzo ya ‘Best Promising Actress.’  Clarice ni mkenya ambaye alipata upenyu kwenye tasnia ya uigizaji nchini Marekani pia ameigiza kwenye movies nyingi za Nigeria.


Post a Comment

 
Top